Sunday, August 30, 2009

SAUTI YA MLA VUMBI




IPO SIKU VUMBI ITAKWISHA NCHI HII .

Tuesday, August 25, 2009

Tanroad wapongezwe!


Mimi binafsi nadhubutu kuipongeza na kusema wanastahili kupewa pongezi kwa kazi zao nyingi wanafanya , kwa kweli wanajitahidi sana , pamoja na vikwazo ambavyo vinaweza kuwa vinawakwaza njia ni kupambana navyo kwa kwa kadri iwezekana maana , Nchi yetu inahitaji maendeleo makubwa ya barabara !

Mfumo mzuri unaleta maendeleo makubwa mno katika kukuza uchumi wa taifa letu ukizingatia tunategemewa na nchi nyingi zilizo pembeni mwetu

Ahsante Wakara wa barabara ongeza bidii kwa ubunifu zaidi .

Monday, August 24, 2009

wanafunzi 12 waunguzwa na moto IRINGA vijijini

Wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodi inayomilikiwa na serikali, iliyopo Tarafa ya Idodi, Iringa Vijijini mkoani Iringa, wamefariki na kuteketea kabisa kwa moto baada ya bweni walimokuwa wamelala kuangamizwa kwa moto. Wanafunzi hao ambao ni wasichana, wamepoteza maisha usiku wa kuamkia jana baada ya chumba kimojawapo cha bweni la wasichana (Nyerere Hostel), kushika moto kisha bweni zima kuteketea. Katika tukio hilo la kusikitisha, wanafunzi wengine 22 wamejeruhiwa, kati yao 14 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na wanane wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Idodi. Shule hiyo ipo katika Jimbo la Ismani linaloongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabone alithibitisha kupokea miili ya marehemu na majeruhi wa ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Umati mkubwa wa wananchi wa Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake, mapema jana asubuhi ulifurika nje ya chumba cha kulaza wageni cha hospitali hiyo baada ya kupata taarifa za ajali hiyo na kufikishwa kwa miili ya marehemu hao ambayo hata hivyo haitambuliki baada ya kuunguzwa vibaya na moto huo. Katika tukio hilo, wanafunzi wengine 427 walinusurika kupoteza maisha yao baada ya jitihada za walimu na wananchi waliowahi kufika katika eneo la tukio, kuanza kuvunja madirisha ili kuwawezesha wanafunzi hao kupata sehemu za kupita na hatimaye kuokoa maisha yao. Bweni hilo lililoteketea kwa moto, lina vyumba 25 na lina uwezo wa kulaza wanafunzi 461 na kwamba wakati moto unashika chumba kimojawapo, wanafunzi hao walikuwemo kwenye bweni hilo. Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa shule hiyo zimesema kulikuwepo na mifupa ya marehemu hao katika lango kubwa la kutokea na inadaiwa kuwa wanafunzi hao huenda walikufa kabla kwa kukanyagwa na wenzao katika harakati za kujiokoa. Ofisa Elimu wa Mkoa wa Iringa, Salum Maduhu na Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Evarist Mangalla, walisema chanzo cha ajali hiyo ni moto wa mshumaa kushika godoro na kuwaka katika chumba hicho. Kwa mujibu wa Kamanda Mangalla, mshumaa huo uliwashwa na mwanafunzi, Naomi Mnyali wakati akijisomea, lakini baadaye alipitiwa na usingizi na kuuacha ukiwaka kabla ya kushika kwenye godoro. Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Kamanda huyo wa Polisi ilisema, mwanafunzi huyo alinusurika katika tukio hilo japo haikuelezwa hali yake ikoje. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Mangalla aliwataja marehemu katika ajali hiyo kuwa ni Matilda Mtewele, Adelvina Kwama na Elizaberth Mtavila ambao walikuwa wanasoma Kidato cha Kwanza. engine ni Digna Ndunguru, Chake Kuyaa, Seciliana John, Lazia Kihwele, Witness Mbilinyi na Stellah Mwigavilo waliokuwa wanasoma Kidato cha Pili. Pia wamo Falha Abdallah na Jesca Wissa waliokuwa Kidato cha Tatu na Maria Ndole wa Kidato cha Nne. Kamanda Mangalla alisema kutokana na marehemu hao kuteketea kiasi cha kutotambulika, wametumia njia nyingine kupata majina yao. Majeruhi wa ajali hiyo mbaya ni Mwizarubi Eliasi, Lucy Sawani, Faraja Sodike, Anoda Ambali, Lela Mkuya, Prisca Melele, Evamary Carlos na Sabrina Abdulrahaman. Wengine ni Lenna Barugu, Zuhra Mazora, Veronika Nyamule, Theresia Zuvapi, Esther Zayumba, Ando Mamba, Irene Mponzi, Ares Ndaga, Lucy Luvanda, Upendo Nyamadule, Fraja Palinoo na Helena Mapunda. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza alithibitisha pia kutokea kwa vifo hivyo akiwa Iringa ambako aliwasili jana asubuhi akitokea Songea mkoani Ruvuma kikazi. “Ni kweli bweni moja katika shule ya Idodi , Iringa Vijijini, limeshika moto usiku wa kuamkia leo (jana) na wanafunzi kumi na wawili wamekufa na wengine kama ishirini na tano wamejeruhiwa. “Niko hapa shuleni tangu asubuhi, hivi sasa tuko katika kikao na uongozi wa Mkoa, Shule na Wazazi kuzungumzia namna ya kufanya maziko,” alisema Mahiza alipozungumza kwa mara ya kwanza na gazeti hili saa 10:32 jioni. Alisema kikao hicho ndicho kilikuwa kikijadili namna ya maziko ya wanafunzi hao 12; kama wazikwe katika kaburi moja au kila familia ikaandae mazishi yake. Lakini baadaye, Mahiza alilieleza gazeti hili kuwa wamekubaliana kwamba maziko ya wanafunzi hao yafanyike kesho saa nane mchana shuleni hapo kwa kufuata taratibu za dini zote kubwa mbili; Kiislamu na Kikristo na uongozi wa Mkoa wa Iringa utatafuta eneo hilo la kuzikia. Kuhusu kutambuliwa kwa marehemu wakati miili yao ilikuwa imeteketea kabisa kwa moto, Mahiza alisema, “Tumetumia kitabu cha majina ya wanafunzi kuwaita walioko hosteli, waliokuwa wamelazwa hospitali ya mkoa na wale waliokuwa katika kituo cha afya Idodi. Kwa hiyo, tukaamini kabisa wale ambao hawapo hata majumbani, ndio waliofariki.” Mahiza, ambaye wakati akizungumza na gazeti hili, alisema Waziri wake, Profesa Jumanne Maghembe alikuwa anaingia mjini Iringa, alisema shule hiyo iliyoko takribani kilometa 108 kutoka Iringa Mjini katika barabara ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ni ya kata na ina wanafunzi wa kike na wa kiume. Mwalimu wa Idodi aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kwa kawaida wanafunzi hutakiwa kuzima taa za umeme wa jenereta ifikapo saa sita usiku, lakini limekuwa jambo la kawaida kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea kujisomea kutumia mishumaa au taa za mafuta. Wanafunzi zaidi ya 400 hawana mahali pa kuishi kutokana na ajali hiyo, na jana jioni, mfanyabiashara maarufu wa Iringa, Salum Abri wa Kampuni ya Asas Dairies alijitolea msaada wa mablanketi 200 na magodoro 200 ili kunusuru vijana walionusurika katika ajali hiyo. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametuma salamu za rambirambi na pole kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari ya Idodi waliothibitishwa kufariki dunia, kutokana na ajali ya moto iliyotokea shuleni hapo usiku wa kuamkia jana. Katika salamu hizo, Waziri Mkuu alisema, kwa niaba ya serikali na kwa niaba yake binafsi, amesikitishwa na kuhuzunishwa sana na tukio hilo na vifo hivyo na kuwaomba wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu na wavute subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. litaka waliojeruhiwa katika tukio hilo watibiwe vizuri ili wapate ahueni haraka. Ajali za moto katika shule nchini zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika miaka ya karibuni, huku mojawapo ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni iliyotokea mkoani Kilimanjaro, katika Shule ya Shauritanga wilayani Rombo mwaka 1994 na kupoteza maisha ya wasichana 43.
Yatufaaa kuwa makini zaidi na ajali za moto hapa nchini ,Ni hatari .
Mungu Tusaidie na ajali hizi

Moto Mashuleni Jamani ,INAUMAA KULIKO maeelezo.


nasikitisha , inauma watoto wetu wadogo zetu kuona wanateketea namna hiii

Tupange mikakati imara na madhubuti na Ajali hizi !
moto ulitokea Idodi secondary inabidi liwe somo kubwa sana ,


Sunday, August 23, 2009

Ajali za pikipiki mjini !




Wandugu wapenzi tuwe makini na vijana hawa waendesha pikipiki hapa mjini maana namna hii zitatuvunja miguu !


kila mtu kwa nafasi yake tujitahidi kuwaelisha vijana ili waweze kuendesha pikipiki kwa uangalifu wa hali ya juu na kutoingia barabara kuu maaana


matukio mengi ya ajali yanatisha ni kwa kuwa basi hatuna mratibu maaalum wa kutoa habari na matukio ya biashara ya pikipiki hapa Dar es salaam , sijui na kwenginepo


mimi binafsi natumi usafiri huu , kwa kuwa ni nrahisi na nafuu ila madhara yake kwa vijana wanatumia barabara pamoja na watumiaji wengine kwa kweli inasikitisha sana maana kila siku ajali ,achilia na matukio ya wizi, wa kuibiana pikipiki ,


Kwa ujumla swala la pikipiki inabidi liwe na sheria maana za kudhibiti matukio kama haya


.


Friday, August 21, 2009

Hii ni haki kweli ?


KWELI DUNIA NA MALIMWENGU HUYO MKIMBIAJI WA AFRIKA KUSINI AMENYIMWA USHINDI WAKE KWA KUHISIWA KUWA NI MVULANA WAKATI YEYE ANAKIMBIA MBIO ZA WANAWAKE !

HAPA KUNA UTATA , ILA SIONI BUSARA KUMZUIA KUPATA MEDALI YAKE BADALA YAKE ANGEPEWA HALAFU AKACHUNGUZWA BAADAE.NA KWA UTARATIBU MAALUMU NA KUFANYA SIRI ILA KWA AINA HII WALIVYOFANYA MIMI SIONI JAMANI SAHIHI JAMANI

Tuesday, August 18, 2009

zombe nje !

Kuachiwa kwa mheshimiwa zombe ndo kumeleta mijadala kibao hapa mjini watu wanajadili kila mahala .

toa mawazo yako !unaonaje wewe mdau kuhusu mwenendo mzima ?

Monday, August 17, 2009

life contents

1 Meaning of life as a question
2 Scientific inquiry and perspectives
2.1 Psychological significance and value in life
2.2 Origin and nature of biological life
2.3 The Big Bang and humanity's fate in this universe
2.4 Scientific questions about the mind
3 Philosophical perspectives
3.1 Ancient Greek philosophy
3.1.1 Platonism
3.1.2 Aristotelianism
3.1.3 Cynicism
3.1.4 Cyrenaicism
3.1.5 Epicureanism
3.1.6 Stoicism
3.2 Enlightenment philosophy
3.2.1 Classical liberalism
3.2.2 Kantianism
3.3 19th century philosophy
3.3.1 Utilitarianism
3.3.2 Marxism
3.3.3 Nihilism
3.4 20th century philosophy
3.4.1 Pragmatism
3.4.2 Existentialism
3.4.3 Absurdism
3.4.4 Secular humanism
3.4.5 Logical positivism
3.4.6 Postmodernism
3.4.7 Naturalistic pantheism
4 Religious perspectives
4.1 Western religions (origins in the Middle East)
4.1.1 Zoroastrianism
4.1.2 Judaism
4.1.3 Christianity
4.1.4 Islam
4.1.5 Bahá'í Faith
4.2 South Asian Religions
4.2.1 Hindu philosophies
4.2.1.1 Advaita and Dvaita Hinduism
4.2.1.2 Vaishnavism
4.2.2 Jainism
4.2.3 Buddhism
4.2.3.1 Early Buddhism
4.2.3.2 Mahayana Buddhism
4.2.4 Sikhism
4.3 Far Eastern Religions
4.3.1 Shinto
4.3.2 Taoism
4.3.3 Confucianism
4.3.4 New religions
5 The meaning of life in popular culture
5.1 Popular views
5.1.1 ...to realize one's potential and ideals
5.1.2 ...to achieve biological perfection
5.1.3 ...to seek wisdom and knowledge
5.1.4 ...to do good, to do the right thing
5.1.5 ...to attain spiritual enlightenment
5.1.6 ...to love, to feel, to enjoy the act of living
5.1.7 ...to have power, to be better
5.1.8 One should not seek to know and understand the meaning of life
5.1.9 Life has no meaning
6 See also
6.1 Origin and nature of life and reality
6.2 Value of life
6.3 Purpose of life
6.4 Miscellaneous
7 References
8 External links
8.1 General
8.2 Scientific
8.3 Philosophical
8.4 Spiritual

Life Ministry


This article is about the philosophical concept of the meaning of life. For other uses, see Meaning of life (disambiguation).

Where Do We Come From? What Are We? Where Are We Going?One of Post-Impressionist Paul Gauguin's most famous paintings.
The meaning of life constitutes a philosophical question concerning the purpose and significance of human existence. This concept can be expressed through a variety of related questions, such as Why are we here?, What's life all about? and What is the meaning of it all? It has been the subject of much philosophical, scientific, and theological speculation throughout history. There have been a large number of answers to these questions from many different cultural and ideological backgrounds. Albert Camus observed, we humans are creatures who spend our lives trying to convince ourselves that our existence is not absurd. [1]
The meaning of life is deeply mixed with the philosophical and religious conceptions of existence, consciousness, and happiness, and touches on many other issues, such as symbolic meaning, ontology, value, purpose, ethics, good and evil, free will, conceptions of God, the existence of God, the soul, and the afterlife. Scientific contributions are more indirect; by describing the empirical facts about the universe, science provides some context and sets parameters for conversations on related topics. An alternative, human-centric, and not a cosmic/religious approach is the question "What is the meaning of my life?" The value of the question pertaining to the purpose of life may be considered to be coincidal with the achievement of ultimate reality, if that is believed by one to exist.